Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV kila siku ya Jumanne saa tatu usiku, umma wa Watanzania walipata kufahamu kilichomkuta binti Emma Roberts. Kwa kukumbusha tu, Emma ni binti aliyefukuzwa shule kutokana na ujauzito. Ujauzito wa Emma ulikuja baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili cha ubakwaji. Kwa mdomo wake mwenyewe, Emma ameelezea hali halisi na kusema kwamba hakupenda huo ndio uwe mustakabali wake wa maisha kwa kuwa alikuwa na ndoto nyingi sana katika maisha.



Bofya hapa